Kuandaa Siku ya kumbukumbu ya Mwanzilishi wa Skauti Duniani
Chama
cha Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam kupitia Kikao chake cha Kamati ya
uendeshaji kimetoa wito kwa Skauti Mkoa wa Dar es Salaam kujiandaa na
siku ya kumbukumbu ya mwanzilishi wa Skauti Duniani (Founder's Day)
inayotarajiwa kufanyika kimkoa kuanzia tarehe 21 Februari, 2014 mpaka 23 Februari, 2014.
"Wito unatolewa kufanya kazi za huduma kwa jamii kwa kujitolea kama ilivyo ada na wajibu wa Skauti" alisema Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Kamishna Abubakar Mtitu. Ndugu Mtitu alisisitiza kuwa Skauti ni watu wenye nidhamu, kujali na kufuata misingi ya utu, kujitoa kwa jamii katika kutekeleza kanuni na ahadi za Skauti.
Pia Kamishna Mtitu alisema mambo waliojadiliana katika kikao hicho ni muhimu sana katika kuendeleza Skauti na wanakamati wamekubaliana kutekeleza maazimio ya kikao hicho.
Mwanyato James ambaye ni Mratibu wa Mafunzo Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam
alisema katika mahojiano na waandishi wa habari kuwa "Natumai
tutayatimiza yote tuliyoyajadili, pia nafuraha sana kuona kikao hiki
kimehudhuliwa na watendaji wakuu wote wa Skauti Wilaya za Dar Es Salaam,
naomba tuendelee hivi kwa kasi hii kwa maendeleo ya Skauti na jamii
yetu"
Kamati imekubaliana kuandaa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa Skauti Duniani (Founder's Day), Marehemu Paden Pawell aliyezaliwa tarehe 12 Februari 1857 na kufariki tarehe 8 Januari, 1941.
Mwenyekiti Mtitu alitumia fursa katika kikao hicho kuwatambulisha baadhi ya wajumbe wapya ambao ni James Mwanyato (Mafunzo), Mama Ramadevi Sankran Lyer (Kabu), Sameer Somji (Kazi Maalum), Titto Jackson pamoja na Leonard Gerlad Kiloka (Uakilishi wa Vijana) na wengine ni S. Salim (Mambo ya Nje na uhusiano), Reuben Mlay (Vijana), Anthony Meda (Makambi na Mawasiliano) na Bi Annick Verstraelen (Miradi)
"Wito unatolewa kufanya kazi za huduma kwa jamii kwa kujitolea kama ilivyo ada na wajibu wa Skauti" alisema Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Kamishna wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Kamishna Abubakar Mtitu. Ndugu Mtitu alisisitiza kuwa Skauti ni watu wenye nidhamu, kujali na kufuata misingi ya utu, kujitoa kwa jamii katika kutekeleza kanuni na ahadi za Skauti.
Pia Kamishna Mtitu alisema mambo waliojadiliana katika kikao hicho ni muhimu sana katika kuendeleza Skauti na wanakamati wamekubaliana kutekeleza maazimio ya kikao hicho.
Mratibu Mafunzo wa Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam Ndugu Mwanyato James |